1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Coca-Cola kuwekeza dola bilioni 1 Nigeria

20 Septemba 2024

Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola inapanga kuwekeza dola bilioni 1 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwenye shughuli zake nchini Nigeria.

Bango la Coca-Cola
Bango la Coca-ColaPicha: DR

Hayo yameelezwa na Rais Bola Tinubu baada ya mkutano na mkurugenzi na mkuu wa fedha wa Coca-Cola, Zoran Bogdanovic, na maafisa wengine kadhaa wa kampuni hiyo.

Bogdanovic amemwambia Tinubu kwamba tangu mwaka 2013, Coca-Cola imewekeza dola bilioni 1.5 nchini Nigeria ili kutanua uwezo wa uzalishaji, kuboresha ugavi pamoja na kwenye sekta ya mafunzo na maendeleo.

Soma zaidi: Mafuriko yasababisha vifo 30 Nigeria

Nigeria, yenye wakaazi zaidi ya milioni 200 inachukuliwa kama soko muhimu kwa makampuni mengi ya kimataifa, lakini matatizo ya kubadilisha fedha za kigeni, urasimu na mikanganyiko ya sera vimekuwa vikiwakatisha tamaa baadhi ya wawekezaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW