1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cologne kumkosa Mark Uth dhidi ya Dortmund

Josephat Charo
15 Agosti 2023

Cologne italazimika kucheza mechi ya ufunguzi ya ligi kuu ya kandanda ya Ujrumani, Bundesliga, bila mshambuliaji wake Mark Uth.

BG Bundesliga Transfers | Mark Uth
Picha: Uwe Kraft/imago images

Cologne itakosa huduma za mshambuliaji wake Mark Uth wakati wa mechi yao ya ufunguzi ya Bundesliga ugenini dhidi ya Borussia Dortmund Jumamosi katika dimba la Signal Iduna Park.

Uth ambaye alikosa msimu mzima uliopita kutokana na uvimbe kwenye mfupa wa nyonga, alipata jeraha kwenye paja wakati wa mechi ya duru ya kwanza ya kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal dhidi ya timu ya daraja la pili VfL Osnabrück. Cologne ilifanikiwa kusonga mbele katika duru ya pili kwa ushindi wa 3-1 katika muda wa ziada.

"Tunaweza kusema kwamba Mark hatacheza wikendi," kocha Steffen Baumgart alisema. "Ni jambo tulilolitarajia. Ukiwa nje ya uwanja kwa mwaka mzima, unahitaji muda kuzowea tena kasi na nguvu ya mchezo."

mshambuliaji wa Cologne, Davie Selke, pia alipata jeraha kwenye msuli wa kwenye paja wakati wa mechi hiyo, lakini Baumgart ana matumaini atakuwa amepona kuweza kucheza mechi ya Jumamosi. "Yeye pia alihisi maumivu makali kwenye paja lake," kocha huyo alisema.

Baumgart alikosoa kwamba timu za daraja la kwanza na la pili zimejipanga kutokucheza mechi za Jumatatu, "lakini sisi tulicheza Jumatatu." Mpinzani wetu anayefuata hakuwa tu na timu rahisi ya kushindana nayo, bali pia siku mbili za kujiandaa. Hili ni jambo linalonikasirisha," Baumgart alisema.

Borussia Dortmund iliicharaza timu ya daraja la nne Schott Mainz 6-1 Jumamosi iliyopita katika mechi ya kombe la shirikisho.

(dpa)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW