1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Waislamu wa Ujerumani wamelaani mashambulio ya treni

26 Agosti 2006

Mashirika makuu 16 ya kiislamu nchini Ujerumani, yamelaani vikali mashambulio mawili ya bomu yaliotaka kufanywa kwenye treni na kushindwa kufanikiwa tarehe 31 Julai.Hati iliyotiwa saini na mashirika yote 16 imesema,mashambulio hayo hayawezi kuhalalishwa kwa jina la uislamu na ugaidi ni kitisho kwa binadamu na pia ni uhalifu dhidi ya wanadamu kwa jumla.Hati hiyo ikaongezea kuwa njama ya mashambulio hayo imewaathiri Waislamu wa Ujerumani wanaolaumiwa na wengi kwa sehemu fulani.Wakati huo huo wanasiasa wa serikali ya muungano nchini Ujerumani wamewataka waislamu nchini Ujerumani washughulike zaidi kuchukua hatua za kuzuia siasa kali miongoni mwao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW