1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiColombia

Colombia: Wazazi wa mwanasoka Luis Diaz watekwa nyara

30 Oktoba 2023

Zaidi ya wanajeshi 120 wa Colombia wakiungwa mkono na polisi wanaendelea kumsaka baba wa mwanasoka nyota wa Liverpool Luis Diaz, aliyetekwa nyara kaskazini mwa nchi hiyo akiwa na mkewe.

Gelsenkirchen Freundschaftsspiel Deutschland Kolumbien
Mwanasoka nyota wa Liverpool na raia wa Colombia Luis DiazPicha: kolbert-press/IMAGO

Wazazi wa mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 26 ambao ni Luis Manuel Diaz na Cilenis Marulanda, walitekwa nyara na watu wenye silaha siku ya Jumamosi katika kituo cha mafuta katika mji wa La Guajira, lakini Mama wa mchezaji huyo aliweza kuokolewa  na polisi saa chache baadaye.

Rais wa Colombia Gustavo Petro  amesema juhudi za kumtafuta baba wa Luiz Diaz zinaendelea huku jeshi likitangaza kuweka vituo vya ukaguzi na kutumia helikopta pamoja na ndege maalum katika zoezi hilo.

Luiz Diaz aliyesajiliwa na klabu hiyo ya Uingereza mwaka 2022 kwa euro milioni 60, hajazungumza chochote juu ya tukio hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW