COLOMBO: Boti za Tamil Tigers zimezamishwa
29 Machi 2007Matangazo
Kwa mujibu wa jeshi la Sri Lanka,wanamaji wamezamisha boti tatu za waasi wa Tamil Tigers nje ya pwani,kaskazini-mashariki ya nchi na si chini ya waasi 15 wameuawa.Shambulio hilo ni mlolongo wa mashambulio ya hivi karibuni katika ardhi kavu na baharini kati ya waasi na vikosi vya serikali nchini Sri Lanka.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili,vimeua kiasi ya watu 68,000 nchini humo.Pande zote mbili sasa zimepuuza makubaliano ya kuweka chini silaha yaliotiwa saini mwaka 2002.