Comoro yalaani tishio la Ufaransa kuhusu msaada
28 Agosti 2026
Matangazo
Akizungumza katika kambi ya jeshi la majini ya Dzaoudzi, Lecornu alisema msaada huo utategemea uwezo wa nchi zinazohusika kuwapokea tena wahamiaji wasio na vibali na kushiriki katika mapambano dhidi ya wasafirishaji haramu wa watu.
Akijibu kauli hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Comoro, Mohamed Mbae, ameiambia AFP kwamba matamshi hayo yalikuwa ya dharau na yasiyovumilika.
Pia amesema kuwa kauli za Lecornu ni za kushangaza na zisizozingatia mahitaji ya wakazi wa Mayotte, ambao bado wanakabiliwa na athari za kimbunga Chido kilichokikumba kisiwa hicho mwaka 2024.
Mayotte ni eneo la Ufaransa lililoko katika Bahari ya Hindi, lakini Comoro bado inalidai kuwa sehemu ya himaya yake. Kauli za Lecornu zimekosolewa pia na makundi mbalimbali ya kisiasa.