Comoro yaweka marufuku ya kutotoka nje usiku
18 Januari 2024Matangazo
Hapo jana jeshi lilifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika Mji Mkuu Moroni ila mapema leo bado waandamanaji walionekana kaskazini mwa mji huo.
Msemaji wa serikali ya Comoro Houmed Msaidie amewalaumu wafuasi wa wagombea wa upinzani walioshindwa uchaguzi kwa maandamano hayo. Msaidie amesema waandamanaji kadhaa wamekamatwa.
Wasiwasi watanda visiwani Comoro baada ya Azali Assoumani kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais
Assoumani ameiongoza Comoro tangu kuingia madarakani kupitia mapinduzi mwaka 1999.
Kulingana na tume ya kitaifa ya uchaguzi, alipata asilimia 62.97 ya kura katika uchaguzi uliopita.