1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY:Rais Conte amteua waziri mkuu mpya Guinea

27 Februari 2007

Rais wa Guinea Lansana Conte hapo jana alimteua balozi wa zamani Lansana Kouyate kuwa waziri mkuu mpya katika kile kinachoonekana kuzingatia matakwa ya vyama vya wafanyikazi nchini humo.

Waziri mkuu mteule ni miongoni mwa watu waliokuwa wamependekezwa kupewa wadhifa huo katika orodha iliyotolewa na vyama vya wafanyikazi pamoja na upande wa upinzani mwishoni mwa juma lililopita.

Lansana Kouyate anachukua mahala pa Eugene Camara ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Conte.

Kuteuliwa kwa Eugene kuliibua ghasia za majuma kadhaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW