CONDOLEEZA RICE NCHINI JAPAN
18 Machi 2005Matangazo
TAARIFA YA HABARI: 11.00 18-03-05
TOKYO:
Waziri wa nje wa Marekani Bibi Condoleeza Rice anatazamiwa kuwasili Japan leo akiwa katika hatua yake nyengine ya zioara yake ya Asia inayolenga kuzungumza na washirika wake juu ya mkakati kuelekea Korea ya Kaskazini.Marekani na Japan zaweza kuzozana juu ya hatu ya Japan ya kupiga marufuku kuagiza nyama ya n’gombe kutoka Marekani.
Mvutano juu ya mradi wa kinuklia wa Korea ya kaskazuini ndio shina la ziara ya Dr.Condoleeza Rice katika ziara yake hii ya kwanza huko Asia tangu kuteuliwa waziri wa nje wa Marekani.
Rice anatarajiwa kukutana na waziri mkuu Koizumi na viongozi wengine wa Japan.