Conte aondolewa mashtaka ya kupanga matokeo
16 Mei 2016Matangazo
Conte ambaye tayari alitumikia adhabu ya kupigwa marufuku miezi minne kuhusiana na kesi hiyo, alituhumiwa kwa kutoripoti tukio la kupanga matokeo yanayohusu mchuano wa ligi ya daraja la pili ya Italia, Serie B mnamo Mei 2011 kati ya timu aliyokuwa akiifunza Siena na ile ya AlbinoLeffe. Kocha huyo wa zamani wa Juventus mwenye umri wa miaka 46, anasisitiza kuwa hakufanya kosa lolote kuhusiana na sakata hilo.
Conte sasa yuko huru kuiongoza Italia katika dimba la mataifa ya Ulaya – Euro 2016 kabla ya kuchukua usukani kuwa kocha wa Chelsea baada ya kukamilika dimba hilo Julai 10.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Yusuf Saumu