1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COP 29 yaingia katika siku ya ziada Azerbaijan

23 Novemba 2024

Mazungumzo ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yameingia katika muda wa nyongeza leo huku yakigubikwa na wingu la hasira na kukatishwa tamaa baada ya washiriki kushindwa kufikia makubaliano,

Aserbaidschan | COP29 UN Klimakonferenz in Baku
Mshiriki akipunga mkono karibu na lango la ukumbi wa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa wa COP29, huko Baku, Azerbaijan Novemba 22, 2024.Picha: Maxim Shemetov/REUTERS

Katika jitihada ya kupata ahadi bora za uchangiaji wa fedha kwa mataifa yaliondelea kwa ajili kukabiliana na athari za kimazingira. Rasimu ya makubaliano ya mwisho ya Jana Ijumaa ilionesha ahadi ya dola bilioni 250 kila mwaka hadi ifikapo 2035, ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya lengo la awali la  dola bilioni 100 lililowekwamiaka 15 iliyopita, kiwango ambacho pia wataalamu walisema kina upungufu wa zaidi ya dola trilioni moja kwa makadirio ya uhitajii Katika nyakati za mapema za Asubuhi ya leo shirika la habari la  The Associated Press liliwashuhudia wapatanishi wakuu kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani na mataifa mengine katika maeneo ya kumbi kadhaa kwa lengo la kufanya mikutano ya kujaribu kuharakisha makubaliano mapya ya mpango huo.