COPENHAGEN: Juhudi za kulinda mazingira ziimarishwe
17 Agosti 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ametoa mwito wa kufanywa bidii zaidi kuhifadhi mazingira. Merkel na Waziri wa Mazingira wa Ujerumani,Sigmar Gabriel wapo katika ziara ya siku mbili kisiwani Greenland,kujionea jinsi mabadiliko ya hali ya hewa duniani,yalivyoathiri kisiwa hicho.
Ongezeko la joto duniani,lilipewa kipaumbele katika ajenda ya mkutano wa kilele wa G-8 ulioongozwa na Kansela Merkel,mjini Heiligendamm miezi miwili iliyopita.