CORD yakataa kuundwa kamati ya Bunge
10 Juni 2016Matangazo
Pande mbili za kisiasa nchini Kenya za CORD na Muungano wa Jubilee zikiendelea kuvutana kuhusiana na kile kinachoelezwa kutokuwa na imani na tume ya kusimamia uchaguzi wa mwakani nchini humo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa kwa upande wao wanatoathimini juu ya mwelekeo wa kisiasa katika kuelekea uchaguzi huo wa mwakani. Baron Shitemi ni mmoja wa wachambuzi hao wa masuala ya kisiasa na amezungumza na Isaac Gamba wa DW.