1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Corona yatishia zaidi ya ajira milioni 20 Afrika

Amina Mjahid
6 Aprili 2020

Umoja wa Afrika umesema nchi za Afrika zitarajie kupoteza mamilioni ya kazi, ongezeko la madeni na mapungufu ya fedha zinazotumwa na raia wake walio nje kama sehemu ya hali ngumu ya kiuchumi kutokana na janga la corona.

Deutschland Flüchtlinge und Arbeit | Flüchtling aus Somalia, Ausbildungsbetrieb
Picha: picture-alliance/dpa/C. Schmidt

Katika utafiti uliochapishwa leo Umoja huo umesema nchi ambazo zinategemea sana utalii na mafuta ndizo zitakazoathirika zaidi.

Ingawa Afrika haijaathirika mno na virusi vya corona kama China, Marekani na Ulaya, inaanza kuhisi athari zake kutokana na uhusiano wa kibiashara wa kanda hizo.

Huku mripuko wa virusi vya corona ukiendelea, kushuka mno kwa bei za mfuta kutaziathiri nchi kama Nigeria na Angola huku marufuku ya kusafiri yakitazamiwa kuigharimu sekta ya utalii ya Afrika dola bilioni hamsini na karibu kazi milioni mbili.