1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Corona yazuwia mkutano mkuu wa Borussia Dortmund 2020

Sekione Kitojo
8 Oktoba 2020

Klabu ya soka  ya Bundesliga  nchini Ujerumani  ya  Borussia Dortmund imeahirisha mkutano wake mkuu  wa mwaka  wa wanachama kwa  muda  usiojulikana  kutokana na  janga la virusi vya corona, klabu hiyo imesema.

Bundesliga - Borussia Dortmund gegen SC Freiburg | Tor Can
Picha: Leon Kuegeler/Reuters

Mkutano  huo  ulipangwa  kufanyika  Novemba 22  lakini rais  wa Borussia  Dortmund, Reinhard Rauball,  amesema  katika  taarifa  ya klabu  hiyo kuwa  kuwa  na  wanachama wengi iwezekanavyo  katika tukio  hilo  hakuwezekani  kutokana  na  vizuwizi, na mkutano  kwa njia  ya  vidio hauwezekani  pia  katika  mwaka  2020.

"Kukiwa  na  karibu  wanachama  160,000 wa  BVB, kwa  bahati mbaya  hakuna  njia  ya  teknolojia  ya  kufanya  mkutano  kama  huo kwa  njia  ya  vidio katika  hali ya inayokubalika," alisema.

"Binafsi nasikitika  kwa  hili,  kwa kuwa  mawasiliano  ya  moja  kwa moja  nanyi, wanachama  wetu, ni muhimu  sana  kwetu."
 

Mkutano  wa  wadau wa  Dortmund kwa wakati huu utafanyika  kwa njia  ya  mtandao, Novemba 19, limesema  gazeti la Kicker.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW