1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Costa: Hatukubali Marekani kuingilia siasa za ndani ya Ulaya

8 Desemba 2025

Rais wa Umoja wa Ulaya Antonio Costa amepinga jaribio lolote la Marekani la kuingilia siasa za Ulaya, baada ya Washington kuchapisha mkakati wa mpya wa usalama, unaokosoa vikali sera za bara hilo.

 Bosnia na Herzegovina | Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa akiwasili katika Kituo cha Ukumbusho cha Srebrenica huko Potocari, Bosnia, Ijumaa, Julai 11, 2025.
Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa akiwasili katika Kituo cha Ukumbusho cha Srebrenica huko Potocari, Bosnia, Ijumaa, Julai 11, 2025.Picha: Armin Durgut/AP Photo/picture alliance

Costa amesema mjini Brussels kwamba ingawa ni kawaida kwamba Marekani na Ulaya hazina maono sawa kuhusu masuala mengi, lakini kitisho cha kuingiliwa siasa za ndani hakikubaliki.

Ametolea mfano wa tofauti ya maono kuhusu uhuru wa kujieleza kati ya Marekani na Ulaya na kusema hakuwezi kuwa na uhuru wa kujieleza ikiwa uhuru wa wananchi kupata taarifa utapindishwa ili kuwalinda watu wa tabaka la juu kama ilivyo nchini Marekani. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW