Cote d'Ivoire yaahidi uchaguzi huru na wa haki
30 Julai 2020Matangazo
Uchaguzi unaonekana kuwa mtihani mkubwa wa udhabiti uliopatikana tangu kulipotokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo ambavyo vilisababisha kuuwawa kwa watu 3,000 katika mwaka 2010 na 2011.
Mzozo kuhusiana na ushindi wa Ouattara katika uchaguzi wa mwaka 2010 ulizusha mzozo na vyama vya upinzani vinashuku kwamba ofisi za tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inamuunga mkono Ouattara.
Tume ya taifa ya Uchaguzi inapanga kufanya mageuzi katika ofisi zake na kushauriana na vyama vyote katika wakati wa kuelekea katika uchaguzi, rais wa tume hiyo Ibrahime Coulibaly Kuibert, aliliambia shirika la habari la Reuters.