1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cote d'Ivoire yaanza mazungumzo na wanajeshi

9 Januari 2017

Waziri wa ulinzi wa Cote d'Ivoire Alain-Richard Donwahi amewasili katika mji wa Bouake kukutana na wanajeshi walioanzisha mgomo ambao umeenea katika taifa hilo la Afrika Magharibi

Elfenbeinküste Bouake Unruhen
Picha: Reuters

Donwahi amesema ametumwa na rais kukutana na wanajeshi hao na kuwasikiliza kwa lengo la kupata suluhisho. Mgomo wa wanajeshi ulioanzia mjini Bouake jana Ijumaa ulienea hadi mji wa Man ulioko magharibi mwa Cote d'Ivoire.

Serikali imesema kuwa wanajeshi hao wanataka kuongezwa mshahara, na kuharakishwa utaratibu wa kuwapandisha vyeo. Ingawa rais Alassane Ouattara amekwenda nchini Ghana katika sherehe za kumwapisha rais mpya, anatarajiwa kurejea nchini jioni. Kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kimeitishwa kujadili mgomo huo wa wanajeshi.

Mwaka 2014 serikali ya Cote d'ivoire ilitumia fedha kuwatuliza wanajeshi waliokuwa wamefanya mgomo kama huu mjini Bouake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW