Cote d'Ivoire.
26 Desemba 2010Kiongozi aliyepo madarakani hivi nchini Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo, amekataa kwa kutaja kutokuwa haki, tishio la viongozi wa mataifa ya jumuiya ya Afrika magharibi la kumuondoa kwa nguvu.
Ijumaa Viongozi wa jumuiya ya kibiashara ya mataifa ya Afrika magharibi , ECOWAS walionya kwamba iwapo Gbagbo hatompisha mpinzani wake Alassane Outtara, basi hawataondoa uwezekano wa kutumia nguvu. Hilo lilikuwa tishio la kwanza la moja kwa moja la kuingiliakati kijeshi, la mataifa ya nje katika mkwamo huo wa uchaguzi, ambao kiasi ya watu 200 wameuwawa.
Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika, na ECOWAS, zote zimetambua matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yaliyoonyesha kuwa Outtara ndie mshindi wa uchaguzi huo wa Novemba. Wakati huo huo kiasi ya watu 14,000 wamekimbia nchini Cote d'Ivoire kuelekea nchi jirani ya Liberia, kutokana na wasiwasi kwamba mzozo huo wa uchaguzi utazusha mapigano ya ndani.
Mwandishi Maryam Abdalla/RTRE
Mhariri:Sekione Kitojo.