1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COTONOU: Kwa mujibu wa ripoti rasmi kiasi watu 113 wamefariki

27 Desemba 2003
kwa ajali ya ndege ya shirika la Libanon nchini Benin. Abiria 22 miongoni mwa 161 wamenusurika, kama ilivyoarifu wizara ya mambo ya kigeni. Abiria wengi Walibanon ambao walikuwa wakirudi nyumbani. Ndege BOEING 727 ya shirika la UTA la Libanon ilikuwa ikielekea Beirut Alhamisi, ilipoangukia baharini ilipoanza kupaa. Vyombo rasmi vya habari vya libanon vimearifu shirika hilo jipya UTA halijapata liseni nchini Libanon, kwa sababu halikutekeleza kikamlifu masharti ya kiufundi. Kampuni hiyo badala ikajiandikisha nchini Guinea.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW