1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COTONOU: Uchunguzi wa ajali ya ndege kuendelea

28 Desemba 2003

Uchunguzi zaidi wa ajali ya ndege ya abiria iliyoanguka majuzi nchini Benin bado unaendelea ambapo taarifa za karibuni zikitaja kuwa boksi la pili la kumbukumbu za usafiri wa ndege hiyo limepatikana. Ndege hiyo ya Boeing 727 ilianguka alhamisi kwenye pwani ya nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi ikiwa katika msafara wa kuelekea Beirut. Watu wasiopungua 130 wamefariki dunia, wengi wao raia wa Lebanon waliokuwa katika safari ya kurudi nyumbani kwa sikukuu za mwisho wa mwaka. Watu wengine 21 walisalimika katika ajali hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW