1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Covid-19 yaongeza vurugu dhidi ya wakimbizi wanawake

21 Oktoba 2020

Wakimbizi wanawake wanasema ukatili dhidi yao umeongezeka kutokana na janga la maambukizo ya Corona katika nchi za Afrika. Uchunguzi umebainisha kwamba ukatili huo umeongezeka kwa zaidi ya asimilia 70, miongoni mwao.

Uganda Flüchtlingslager Palorinya Südsudan
Picha: DW/L. Emmanuel

Wanawake zaidi ya 850 waliohojiwa kwenye nchi 15  za Afrika kulingana na uchunguzi wa kamati ya kimataifa  ya uokozi IRC. Thuluthi moja ya akina mama hao wameshuhudia ongezeko la ndoa za kulazimishwa.

Hatua za karantini zilizochukuliwa kwa lengo la kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona duniani kote zimesababisha mlipuko wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo wanawake hao wanalazimika kutumia muda zaidi pamoja na wale wanaowanyanyasa katika namna kwamba wanawake hao wanashindwa kujihami.

Soma pia: Uganda yakataa kuwahifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini

Mashirika ya kutetea haki za wanawake na wasichana yanasema shida za kiuchumi na kijamii zinazofanywa kuwa mbaya Zaidi kutokana na hatua za karantini zinazababisha wanawake na wasichana wawe wahanga kwa urahisi.

IRC inasema fedha ni haba kwa ajili ya kuwasaidia mamilioni ya wakimbizi, wanawake na wasichana ambao hasa ni rahisi kuwa wahanga.Picha: picture-alliance/AP Photo/R. Gul

Kutokana na familia kushindwa kukidhi mahitaji kwa sababu ya kutokuwa na vipato, wasichana wengi wanalazimika kujiuza kwa ajili ya kupata fedha za kununulia chakula au wanalazimishwa kuolewa ili kupunguza mzigo wa gharama kwenye familia zao.

Licha ya kadhia hizo, kamati ya kimataifa ya uokozi, IRC imesema fedha ni haba kwa ajili ya kuwasaidia mamilioni ya wakimbizi, wanawake na wasichana ambao hasa ni rahisi kuwa wahanga.

Soma pia: UNHCR yafunga shughuli katika kituo cha wakimbizi Tripoli

Jamii ya kimataifa yaendelea kupuuza tatizo

Mkurugenzi mwandamizi wa kamati hiyo ya kuzuia ukatili wa kijinsia Nicole Behnam amesema licha ya tahadhari zilizotolewa mapema kutokana na tajiriba za wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, jumuiya ya kimataifa inaendelea kupuuza ukatili huo.

Uchunguzi uliofadiliwa kutokana na msaada wa Ireland ulifanywa kwa kuwahoji wanawake katika nchi kadhaa za Afrika ikiwa pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia  ya Kongo, Uganda, Chad, Cameroon, Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini. Nchi nyingine ni Nigeria na Sierra Leone.

Uchunguzi umebainisha kuwa ukatili umeongezeka kwa zaidi ya asimilia 70, miongoni mwa wakimbizi wa ndani wanawake. Picha: Getty Images/AFP/S. Maina

Wanawake waliohojiwa wamezungumzia juu ya vitisho vya kufukuzwa kwenye nyumba na wamiliki wa nyumba  hizo. Pia wameelezea juu ya kulazimishwa kufanya ngono ili kupata fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula.

Kutokana na mahitaji ya maji wanawake na wasichana wanalazimika kutumia muda mwingi kwenye sehemu za kuchotea maji ambako wanaingia kwenye mitego ya kunyanyaswa kingono.

Soma pia: Amnesty International: Wakimbizi wa ndani nchini Somalia wakabiliwa na dhiki kubwa

Kulingana na ripoti, akina mama hao wanafanyiwa ukatili na wanajeshai na polisi, hasa wakati maafisa hao wanapotekeleza amri ya kutotoka nje.

Uchunguzi pia umebainisha kwamba wasichana wameathirika kutokana na kukosa usalama baada ya shule kufungwa. Hali hiyo imesababisha ndoa za kulazimishwa, ujauzito wa mapema na bughudha za kingono.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa mwito kwa nchi wa kuchukua hatua dhidi ya kuongezeka kwa ukatili wanaofanyiwa wanawake na wasichana mnamo nyakati hizi za janga la corona.

Wahamiaji wa Burundi walioko Tanzania waanza kurejea nyumbani

01:52

This browser does not support the video element.

Kamati ya kimataifa ya uokozi IRC imesema wafadhili wameshindwa kutoa fedha za kutoshMilioni 30 waambukizwa virusi vya corona duniania kwa ajili ya kuwasaidia wale waliomo katika hatari kubwa zaidi na hasa wanawake na wasichana ambao wamelazimika kuyakimbia makaazi yao kutokana na migogoro au majanga ya asili na kuishi ugenini.

Soma pia: UNHCR: Wahamiaji wanyanyaswa na maafisa wa Afrika

Umoja wa Mataifa umetoa mwito wa kuchangisha kiasi cha dola zaidi ya milioni 10 ili kuwasaidia watu hao duniani kote. Hata hivyo hadi sasa kiasi kilichopatikana ni asimilia 30 ya fedha zinazohitajika.

Mkurugenzi mwandamizi wa kamati ya kimataifa ya uokozi Nicole Behnam amesema wakati wa maneno matupu umeshapita na kwamba kinachotakiwa sasa ni hatua thabiti.

Chanzo: RTRE