Cristiano Ronaldo asema Kombe la Dunia la 2026 ni la mwisho
11 Novemba 2025
Matangazo
Nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Al Nasr, Cristiano Ronaldo amesema leo Jumanne kwamba Kombe la Dunia la hapo mwakani litakalofanyika katika nchi za Marekani, Canada na Mexico litakuwa la mwisho.
Hivi majuzi mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40 aliweka rekodi ya kufikisha zaidi ya mabao 950 katika ngazi ya klabu na kimataifa. Nyota huyo ameongeza kwamba atastaafu kucheza kandanda ndani ya kipindi cha mwaka mmoja au miwili ijayo.
Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Oranapambana ili aweze kucheza katika Kombe la Dunia kwa mara yake ya sita. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2006.
Hata hivyo, Ureno bado haijafuzu kwa mashindano ya2026 lakini inaweza kujihakikishia nafasi yao ikiwa itaifunga Ireland siku ya Alhamisi.