Cuba yakubali mikataba ya UN
11 Desemba 2007Matangazo
HAVANA:Cuba imesema kuwa itaridhia mikataba miwili mikubwa ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za kiraia na kisiasa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Felipe Perez Roque amesema kuwa uamuzi huo una nia ya nchi hiyo kuwa na ushirikiano kamili na Umoja wa Mataifa.
Lakini akasema kwa upande mwengine Umoja wa Mataifa nao unawajibika kuheshimu Cuba kama nchi inayojitawala na wananchi wa Cuba wana haki ya kujiamulia mambo yao.
Taarifa imekuja wakati ambapo hapo jana wakati wa maadhimisho ya siku ya haki za binaadamu, wafuasi wanayoiunga mkono serikali waliandamana katika mji mkuu Havana kuipinga siku hiyo.