1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Cuba yakumbwa na giza tena ndani ya wiki moja

22 Machi 2026

Cuba imetumbukia katika giza tena katika kipindi kisichozidi wiki moja kutokana na kushindwa kufanya kazi mfumo wa kuzalisha umeme nchini humo.

Cuba Havanna 2026
Matatizo ya umeme yameongezeka tangu kutekwa nyara rais wa Venezuela Nicolus MaduroPicha: Yamil Lage/AFP

Matatizo ya umeme yameongezeka tangu kutekwa nyara rais wa Venezuela Nicolus Maduro.

Wakati wa utawala wa Maduro, Venezuela ilikuwa mshirika wa Cubana ndio ilyokuwa mtoaji mkuu wa mafuta kwa Cuba. Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuziwekea ushuru nchi zitakazoiuzia mafuta Cuba. 

Wakati huohuo kuna taarifa kwamba meli mbili zenye shehena ya petroli na diseli zipo njiani kuelekea Cuba.

Trump ameeleza wazi kuwa anataka mabadilikom ya uongozi kwenye taifa hilo lenye watu milioni 9.6. Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel amesema uvamizi wowote nchini mwake utakabiliwa kwa nguvu zote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW