Cuba yaomba msaada kuhusu vikwazo vya Marekani
8 Julai 2026
Waziri wa mambo ya nje wa Cuba Bruno Rodriguez amelaani vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya kisiwa hicho cha kikomunisti wakati wa mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa jana Jumanne ambao ulifanyika licha ya shinikizo la kidiplomasia kutoka Marekani kuuzuia.
Rodriguez aliliambia baraza hilo kwamb aserikali ya Marekani inatekeleza vita vya pande nyingi, visivyo vya kawaida dhidi ya Cuba ambavyo tayari vimedumu kwa karibu miongo saba sasa na vimekuwa vya kikatili zaidi katika miezi saba iliyopita.
Rodriguez likosoa adhabu ya pamoja ya kizuizi hicho kwa idadi ya watu. akiongeza kwamba kuzingatia uhalifu huu wa kikatili pia ni jukumu la Umoja wa Mataifa.
Rodriguez alisema uharibifu uliosababishwa na vikwazo hivyo wakati wa kipindi cha Machi 2025 hadi Februari 2026 ni sawa na rekodi ya dola bilioni 8, ongezeko la asilimia saba zaidi ya kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita, akibainisha kuwa takwimu hizo hazijumuishi athari kubwa ya kizuizi cha mafuta ambacho Marekani iliwekea Cuba mwezi Februari.