1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cunha akamilisha "ndoto" ya kujiunga na Man United

12 Juni 2025

Manchester United imethibisha kumsajili kiungo mshambuliaji Matheus Cunha kutoka Wolves kwa mkataba wa miaka mitano, wenye chaguo la kuongezwa mwaka mmoja zaidi.

Bundesliga | Matheus Cunha
Mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil Matheus Cunha amesaini mktaba wa miaka mitano na Manchester United.Picha: Revierfoto/picture alliance

Cunha mchezaji wa kimataifa wa Brazil, alieleza furaha yake, akisema hatimaye ndoto yake ya kuichezea United imetimia. Usajili huu ni wa kwanza kwa Ruben Amorim kwenye dirisha la usajili la majira ya joto, wakati akijaribu kukijenga upya kikosi chake.

Mkurugenzi wa soka wa United, Jason Wilcox, amesema Cunha ana sifa zote wanazotafuta katika azma yao ya kujenga timu yenye nguvu, inayovutia na inayoweza kushindania mataji makubwa.

Nchini Uhispania Beki wa zamani wa Liverpool Trent Alexander-Arnold alitaja uhamisho wake Real Madrid kama "ndoto iliyotimia" wakati akitambulishwa rasmi katika klabu ya La liga.

Hapa Ujerumani Winga Leroy Sané ameandikia ujumbe wa kuaga Mashabiki waBayern Munich kabla ya uhamisho wake unaotarajiwa kuelekea Galatasaray ya Uturuki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW