1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DÜSSELDORF: Waserb wakosolewa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa

27 Agosti 2006
Mjumbe mteuliwa wa Umoja wa Mataifa katika Kosovo,Joachim Rücker ametoa lawama kali dhidi ya Waserb.Katika mahojiano yake na gazeti la “Handelsblatt”,Rücker amesema,viongozi wenye misimamo mikali katika serikali ya Belgrade waache kuweka vizingiti kwa Waserb wa Kosovo kujijumuisha kisiasa na kiuchumi.Kwa sababu hiyo, Wa-Kosovo wenye asili ya Ki-Albania hawawezi kulaumiwa peke yao kwa ukosefu wa kuwajumuisha Waserb walio wachache huko Kosovo.Rücker amepinga kabisa,uwezekano wa kulitenga eneo la kaskazini la Kosovo ambako wakazi wengi ni Waserbia.Mwana diplomasia huyo wa Kijerumani atashika madaraka ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kosovo tarehe mosi mwezi Septemba.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW