DÜSSELDORF:Rais Hu atembelea mkoa wa viwanda
12 Novemba 2005Matangazo
Rais Hu Jintao wa China akiwa mwisho wa ziara yake nchini Ujerumani,amewasili mjini Düsseldorf katika mkoa wa viwanda wa North Rhine Westphalia.Kiasi ya mashirika 150 ya Kichina yana matawi yake katika sehemu mbali mbali za mkoa huu.Rais Hu,mbali na kulitembelea eneo hili la viwanda ameomba pia kukutana na familia moja ya mchimba mgodi.Siku ya jumapili Rais Hu na wajumbe wanaomsindikiza wataelekea Uhispania.