DAKAR : Watoto waendelea kufa njaa Niger
17 Septemba 2005Matangazo
Watoto bado wanaendelea kufa njaa nchini Niger licha ya kurupuko la jitihada za misaada na nadhari ya vyombo vya habari.
Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limesema maelfu bado wanaendelea kukabiliwa na njaa na limeshutumu shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa kwa kuchelewa kuchukuwa hatua na kushindwa kuwasaidia wale wanohitaji msaada kwa haraka.
Michango ya dharura imekuwa ikiongezeka sana katika miezi ya hivi karibuni kutokana na picha za kuhuzunisha za watoto waliokonda na dhoofu wa Niger zilizotolewa na vyombo vya habari duniani.
Operesheni za kusaidia watu milioni 3 na laki sita wanaokabiliwa na njaa hatimae zilipamba moto baada ya miezi kadhaa ya miito ya serikali kuangukia kwenye masikio ya kufa.