1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Muito wa kumuunga mkono al-Assad

10 Machi 2005

Wasyria kwa maelfu wamekusanyika katika mji mkuu Damascus kumuunga mkono rais Bashar al-Assad.Wafanya maandamano hao wameilani hatua ya jumuiya ya kimataifa kuzidi kuishinikiza Syria na wameahidi kuiunga mkono Lebanon.Maandamano hayo yamefanywa siku moja baada ya raia wa Lebanon kwa maelfu kuitikia muito wa kundi la Hizbollah kuandamana mjini Beirut kuiunga mkono Syria.Kwa wakati huo huo vikosi vya Syria vimeanza kuhamia eneo la mashariki la Lebanon,hiyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuviondosha vikosi vya Syria kutoka Lebanon kwa awamu mbili kama ilivyokubaliwa na marais wa Lebanon na Syria siku ya jumatatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW