1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: RAIS ASSAD KULIHOTUBIA BUNGE

5 Machi 2005

Rais Bashar al-Assad wa Syria hii leo analihotubia bunge la taifa ikisemekana kuwa atatangaza hatua ya kuhamishwa sehemu kubwa ya vikosi vya nchi hivyo vilivyokuwepo nchi ya jirani Lebanon.Bado haijulikani ni idadi gani ya vikosi vitakavyohamishwa.Rais Assad anachukua hatua hiyo kufuatia shinikizo la jumuiya ya kimataifa kuwa Syria iwaondoshe wanajeshi wake 14,000 kutoka Lebanon.Syria imezidi kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa baada ya kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafik al-Hariri mwezi uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW