1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damascus. Rais Mubarak azuru Syria

15 Machi 2005

Rais Hosni Mubarak amewasili mjini Damascus , nchini Syria kwa mazungumzo na rais Bashir al Assad. Duru za kidiplomasia zimesema kuwa mazungumzo yalitarajiwa kulenga katika suala la Lebanon.

Ziara hiyo inakuja wakati majeshi ya Syria yaliyoko katika ardhi ya Lebanon yanaondolewa kutoka katika nchi hiyo.

Hadi sasa, zaidi ya wanajeshi 4,000 wa Syria wanaripotiwa kuwa wameondoka Lebanon katika hatua ya kwanza yenye awamu mbili ya kuyaondoa majeshi hayo hatua iliyoanza wiki iliyopita.

Hapo jana , mamia kwa maelfu ya waandamanaji wanaoipinga Syria waliandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Lebanon , Beirut wakidai kufanyika uchunguzi juu ya kifo cha waziri mkuu wa zamani Bwana Rafik Hariri aliyeuwawa mwezi mmoja uliopita. Viongozi wa upinzani nchini Lebanon

Wanaitupia lawama Syria kwa mauaji ya Hariri. Serikali ya Syria imekanusha madai hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW