1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Rais wa Syria, Bashar al-Assad, kuhutubia juu ya azimio la umoja wa mataifa

10 Novemba 2005

Rais wa Syria, Bashar al-Assad anatarajiwa kutoa hotuba yake huku akikabiliwa na shinikizo la umoja wa mataifa kuwaruhusu maofisa wa Syria wa ngazi za juu kuhojiwa na timu ya umoja huo inayochunguza mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon, Rafik Hariri.

Asad anatarajiwa kuzunguzia juu ya azimio la umoja wa mataifa linaloitaka Syria kushirikiana kikamilifu na umoja huo. Maelfu ya wanafunzi wamekusanyika katika chuo kikuu cha Damascus wakiwa wamebeba bendera za Syria wakisubiri hotuba hiyo.

Syria imesema maofisa wake waliotajwa katika kifo cha Hariri, wanahojiwa na jopo maalumu, hivyo hawawezi kuruhusiwa kwenda Lebanon kuhojiwa na timu ya umoja wa mataifa mpaka waruhusiwe na jopo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW