1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria kuhamisha vikosi vyake

6 Machi 2005

Rais Bashar al-Assad wa Syria ametangaza kuwa vikosi vya nchi hiyo vilivyokuwepo Lebanon vitahamishwa.Amesema kwanza vikosi hivyo vitapelekwa mashariki mwa Bonde la Bekaa na baadae kwenye mpaka wa Syria.Lakini hakutaja lini hasa hatua hiyo itachukuliwa.Akilihotubia bunge siku ya jumamosi,Assad alisema kuwa kwa kuvihamisha vikosi hivyo Syria itatimiza wajibu wake wa kimataifa.Syria imezidi kushinikizwa kuondoka Lebanon tangu waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik al-Hariri kuuawa wiki tatu za nyuma.Syria na washirika wa Kilebanon wamelaumiwa kwa mauaji ya Hariri na maandamano makubwa ya umma yaliilazimisha serikali ya Lebanon inayoungwa mkono na Syria kujizulu wiki iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW