1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria tayari kuyaondoa majeshi yake yote kutoka Lebanon.

30 Machi 2005

Syria imetangaza kuwa itayaondoa majeshi yake yote kutoka Lebanon kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo kufanyika.

Waziri wa mambo ya nje wa Syria Faruq al-Shara amesema hayo katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Koffie Annan.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Syria amesema kuwa hadi kufikia sasa Syria imeshawaondoa wanajeshi wake alfu kumi kati ya wanajeshi alfu arubaini nchini Lebanon na kutoa ahadi ya kuwaondoa wanajeshi wake wote kabla ya uchaguzi wa Lebanon unaotarajiwa kufanyika hapo mwezi wa May.

Vuguvugu la kuitaka Syria iyaondoshe majeshi yake kutoka Lebanon lilizidi mwezi uliopita kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri ambapo Syria inalaumiwa kwa kifo chake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW