1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria yakubali maofisa wake wahojiwe na umoja wa mataifa

3 Novemba 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria, Walid Muallem, amesema tume ya umoja wa mataifa inayochunguza mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon, Rafik Hariri, ina uhuru wa kumhoji afisa yeyote wa Syria.

Syria imeuruhusu umoja wa mataifa kuwahoji maofisa waliotajwa au watakaotajwa katika ripoti ya muongoza mashataka wa Ujerumani, Detlev Mehlis. Waziri Muallem hakusema ni wapi maofisa wa Syria watakakohojiwa lakini akathibitisha kwamba Syria itashirikiana na tume ya ndani inayochunguza kesi hiyo kwa kuwa Syria inaamini haikuhusika kwa njia yoyote katika mauji ya Hariri.

Ameongeza kusema kwamba serikali ya Damscus iko tayari kusaini mkataba kati ya tume ya uchunguzi nchini humo na umoja wa mataifa, ikiwa kufanya hivyo kutachangia katika uchunguzi huo.

Wakati huo huo, rais Bashad al-Assad amewaachilia huru wafungwa 190 wa kisiasa katika kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa ramadhani. Hatua hiyo inafanyika wakati rais Assad anapokabiliwa na shinikizo kufuatia ripoti ya uchunguzi wa maauji ya Hariri iliyowataja maofisa kadhaa wa serikali yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW