1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Umoja wa mataifa wataka kuanza kuwahoji washukiwa wa Syria

7 Novemba 2005

Syria imepokea ombi rasmi kutoka kwa tume maalumu ya umoja wa mataifa inayotaka kuwahoji washukiwa wa Syria katika uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon, Rafik Hariri. Serikali ya Damascus inalifikiria ombi hilo lakini afisa wa wizara ya mabo ya kigeni hakuyataja majina ya watu wanaotakiwa kuhojiwa na tume hiyo.

Magazeti nchini Lebanon yamesema mmoja wao ni jenerali Assef Shawkat, shemejiye rais Bashar al-Assad na kiongozi wa ukachero. Ripoti ya uchunguzi wa kifo cha Hariri iliyotolea mwezi uliopita iliitaja Syria kwamba ilihusika katika njama ya mauji ya kiongozi huyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW