DAMASCUS: Vikosi vya Syria vikae tayari
1 Agosti 2006Matangazo
Rais Bashar al-Assad wa Syria ametoa amri kwa vikosi vya nchi yake kukaa katika hali ya tahadhari,wakati mgogoro ukiendelea katika kanda hiyo.Mapema hii leo ndege za kivita za Israel zimeshambulia barabara inayounganisha eneo la kaskazini-mashariki ya Lebanon na Syria.Hivi sasa hakuna habari kuhusu hasara iliyopatikana.
