DAR ES SALAAM : Kituo cha teknolojia ya hali ya juu cha matibabu ya UKIMWI chafunguliwa Tanzania
6 Oktoba 2005Matangazo
Rais Benjamin Mkapa na Mfuko wa Maabara wa Abbott wamefunguwa kituo cha teknolojia ya hali ya juu kwa wagonjwa wa nje wasiohitaji kulazwa na maabara ya uchunguzi katika mji wa D’salaama leo hii kama sehemu ya mpango mkubwa wa kuboresha matibabu ya UKIMWI huko Afrika Mashariki.
Kituo hicho katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pia ni sehemu ya mpango wa taifa zima kuboresha miundo mbinu ya huduma za matibabu nchini Tanzania.
Mfuko wa Abbott kitengo cha ufadhili cha Abbott Park ambayo ni kampuni ya madawa ilioko Illinois nchini Marekani imewekeza dola milioni 35 katika mfumo wa afya nchini Tanzania tokea mwaka 2001.
Uwekezaji huo ni sehemu ya mjadala unaoendelea wa matibabu ya UKIMWI barani Afrika.