1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Marefa 22 wasimamishwa kazi

11 Julai 2007

Shirikisho la soka nchini Tanzania, TFF, limewasimamisha kazi marefa 22 na makamishna wanne wa soka wanaoushutumiwa kwa kuwa na upendeleo kwenye mechi za ligi ya taifa iliyomalizika juzi Jumapili.

Uamuzi uliopitishwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la TFF kufuatia madai ya upendeleo na ulaji rushwa umetangazwa hii leo.

Katibu mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela, amesema adhabu itakayochukuliwa dhidi ya maafisa hao itatekelezwa baada ya uchunguzi wa kina kufanywa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW