DAR ES SALAAM : Meya wa zamani aongezewa kifungo cha miaka 10 zaidi
22 Mei 2005Mahkama ya Umoja wa Mataifa inayowashtaki wapangaji wa mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994 imeongeza hukumu ya meya wa zamani kwa miaka 10 zaidi, imetupilia mbali rufaa yake na kugunduwa kwamba alikuwa hata anawajibika zaidi kwa mauaji yaliyotokea kwenye mji wake.
Hukumu hiyo ya kitengo cha rufaa cha Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Rwanda inaamanisha kwamba Laurent Semanza meya wa zamani mwenye umri wa miaka 61 wa mji wa Bicumbi katika jimbo la vijijini la Kigali lazima sasa atumikie kifungo cha miaka 35 gerezani badala ya 25.
Mahkama imegunduwa Semanza ameamuru kubakwa, kuteswa na kuuwawa kwa Watutsi waliokuwa wamejificha kwenye kanisa ambalo lilikuwa chini ya mamlaka yake.
Semanza alikamatwa nchini Cameroon hapo mwaka 1996 na mwaka uliofuatia alihashimiwa katika kituo cha mahabusu cha Umoja wa Mataifa mjini Arusha.