DAR ES SALAAM: Mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Ruanda ajisalimisha
9 Novemba 2005Matangazo
Mtu anayetuhumiwa kuwa kiongozi katika mauaji ya halaiki ya mwaka wa 1994 nchini Ruanda alijisalimisha katika mahakama ya kimataifa inayosikiliza kesi za washukiwa wa mauaji hayo mjini Arusha.
Callixte Kalimanzira, mwenye umri wa miaka 52, anakabiliwa na mashataka matatu likiwemo mauaji ya halaiki. Anashatakiwa kwa kuwachochea wahutu wenzake kuwaua watutsi, wakiwemo wanawake, watoto na wazee.
Mahakama ya kimataifa mjini Arusha nchini Tanzania, inamzuilia Kalimanzira aliyejisalimisha kwa maofisa nchini humo hapo jana. Kalimanzira aliyekuwa naibu waziri katika serikali ya Ruanda, anashtakiwa pia kwa kugawanya silaha na kusimamia mauaji ya watutsi.