1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Usalama na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu

2 Septemba 2005

Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania ameahidi kuhifadhi usalama na utulivu wakati wa uchaguzi wa mwezi Oktoba,zikiwepo khofu za kuzuka machafuko kisiwani Zanzibar.Katika hotuba yake ya taifa ya kila mwezi kwenye televisheni,Mkapa amesema kampeni za uchaguzi zisiwe jukwaa la kueneza ushindani,chuki au uhalifu.Vile vile katika hotuba hiyo rais Mkapa amekariri msimamo wake kuhusu watazamaji wa uchaguzi wa kigeni.Amesema,watazamaji hao wanakaribishwa mradi hawatojaribu kuingilia mambo ya kisiasa ya Tanzania.Rais Mkapa ambae hawezi kugombea awamu ya tatu,atastaafu baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 30.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW