1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Daresalam: Madhamana wanne wa zamani wa Rwanda watafikishwa...

26 Novemba 2003
mahakamani kesho kuhusika na mauwaji ya halaiki ya mwaka 1994.Wanatuhumiwa kuandaa makundi ya wanamgambo na kutayarisha orodha ya majina ya watu waliobidi kuuliwa."Kesi ina umuhimu mkubwa hasa kwakua inafafanua nafasi iliyoshikiliwa na madhamana wa zamani wa ngazi ya juu serikalini" amesema hayo msemaji wa korti ya kimataifa ya uhalifu wa vita vya Rwanda Roland Amoussouga."Wanatuhumiwa kuandaa mipango kwa ushirikiano pamoja na wengineo,ili kuwateketeza watu wa kabila la tutsi na kuwaangamiza wapingani ili waweze kusalia madarakani."ameongeza kusema msemaji wa korti kuu ya kimataifa.Watuhumiwa hao ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Edouard Karemera na waziri wa zamani wa elimu Andre Rwamakuba,mwenyekiti wa chama tawala cha zamani MRND,Mathieu NGIRUMPATSE na katibu mkuu wake JOSEPH NZIRORERA.Wanatuhumiwa kuhusika na mauwaji ya halaiki,kuchiochea mauwaji,uhalifu dhidi ya ubinadam na uhalifu wa vita.Wote wanne wanakana madai dhidi yao.Kesi hiyo,ya pili ya aina yake ilikua ianze kusikilizwa leo,imeakhirishwa lakini kutokana na uamuzi wa viongozi wa serikali ya Tanzania wa kusherehekea siku kuu ya Idd El Fitr hii leo.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW