DARESALAM: Serikali na waasi wa FNLwatia saini makubaliano ya amani Burundi
16 Mei 2005Matangazo
Hatimaye rais wa Burundi Domitien Ndayizeye na Kiongozi wa Kundi la waasi wa FNL Agathon Rwasa wametia saini makubaliano ya kumaliza mapigano nchini Burundi. Kundi la waasi wa Fnl ndio kundi la pekee nchini Burundi linaloendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya viongozi hao wawili yaliyofayika katika makao ya rais Benjamin Mkapa wa Tanzanuia jijini Daresalam hapo jana.
Pande hizo mbili zinatarajiwa kuanza mazungumzo katika kipindi cha mwezi mmoja kujadili juu ya kupatikana amani ya kudumu nchini Burundi.
Kiasi cha watu laki 3 waliouwawa nchini humo katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliochukua zaidi ya muongo mmoja.