David Cameron ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya nje Uingereza
13 Novemba 2023Matangazo
Cameron pia anatarajiwa kuteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la juu la Bunge la Uingereza.
Cameron ambaye uteuzi wake umewashangaza wengi, alikuwa Waziri Mkuu kutoka chama tawala cha Conservative kati ya mwaka 2010 hadi 2016 alipojiuzulu baada ya kura aliyoishinikiza ya maoni ya Brexit ya mwaka 2016, kuibua ukosoaji mkali.
Mabadiliko haya yanafanyika baada ya Waziri Mkuu Rishi Sunak kumfukuza Waziri wa Mambo ya Ndani Suella Braveman baada ya kukosoa namna jeshi la polisi linavyoshughulikia maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina.
Huku hayo yakiendelea Waziri wa Mazingira Therese Coffey naye amejiuzulu.