1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dawa ya kutuliza masoko, hakuna taifa linaloweza kuwa na dawa ya mzozo huu wa fedha.

6 Oktoba 2008

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa uhakikisho kuwalinda wateja wenye fedha zao katika mabenki nchini Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mwishoni mwa juma ametoa uhakikisho wa kulinda kwa hali yoyote ile fedha walizoweka wateja katika mabenki nchini Ujerumani.

Hii inafuatia mfano wa Irland na Ugiriki na mataifa mengine ya umoja wa Ulaya yamo katika mbinyo.

Andreas Becker katika uhariri wake anasema kuwa hii ni dawa ya muda tu ya kutuliza kisaikolojia.

Msiwe na wasi wasi , fedha zenu ziko salama. Huo ni ujumbe wa wanasiasa wa Ujerumani kwa watu walioweka fedha zao katika mabenki.

Wanatoa uhakikisho sasa kwa usalama wa waliohifadhi fedha zao katika akauti za mabenki ya Ujerumani. Wizara ya fedha imeitaka serikali kutenga zaidi ya Euro bilioni 1,000. Ikiwa lakini watu wote watajaribu kukimbilia kuziondoa fedha zao katika mabenki, kwa kuwa uhakikisho huo hauna thamani kubwa, tarakimu hiyo haitakuwa na maana yoyote.

Kiini cha uhakikisho huo wa serikali pia ni wa kisaikolojia, kutokana na kiwango cha mzozo huo wa kifedha ambao unawatisha wananchi. Kutokana na hayo, ni lazima serikali kutoa uhakikisho, kwa matumaini kuwa serikali itajiepusha, iwapo kutakuwa na madai.

Tatizo hili hata hivyo ni tofauti, hadi sasa katika mzozo huu hakuna benki ya Ujerumani iliyotumbukia katika matatizo haya, ambapo watu walioweka fedha zao wanazitaka.

Kwa upande wake wateja walioweka fedha zao katika benki ya mikopo ya nyumba nchini Uingereza ya Northern Rock walikuwa mlangoni mara baada ya kupata taarifa ya kukaribia kuporomoka benki hiyo.

Kuna sababu mbili zilizosababisha mabenki kuingia katika matatizo haya, ama zina madai mengi ya kifedha katika vitabu vyake, ambayo yako katika msingi wa madeni yasiyolipika ya mikopo ya nyumba nchini Marekani na kulazimika kufutwa. Ama kutoweza kuuzwa kwa haraka mali zake katika masoko ya fedha, kwa kuwa mabenki moja baada ya nyingine kutoaminiana na kwamba kwa wakati huo hayawezi kupeana mikopo.

Uhakikisho wa serikali kwa wateja wenye fedha zao katika mabenki hauondoi tatizo lolote kati ya haya. Ni dawa ya kuzuwia tu hali hii, ambayo mabenki yamejikuta katika hali hii ya kuyumba.

Siku ya Ijumaa kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliishutumu serikali ya Irland, kwa kukingia kifua wateja walioweka fedha zao benki.

Siku chache baadaye amefanya kile kile ambacho serikali ya Ireland imefanya. Kila nchi inapaswa kutoa uhakikisho kama huo, wakati mbinyo unazidi kuwa mkubwa kwa serikali kufanya zaidi. Ama sivyo serikali zinahatarisha kupoteza mitaji ya fedha , kwa wateja kupeleka fedha zao katika nchi nyingine.

Mwishowe , ni muhimu kupatikana jibu la pamoja na Ulaya hata kama serikali hazitaweza kupata msimamo wa pamoja katika mikutano.

Kwanza kabisa sera za fedha za bara la Ulaya ni suala la kitaifa. Lakini hali halisi hivi sasa inaonekana vingine kabisa.

►◄