1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaDenmark

Denmark yaapa kamwe Marekani haitoichukua Greenland

23 Desemba 2025

Viongozi wa Denmark na wale wa kisiwa cha nchi hiyo kinachojitawala chenyewe cha Greenland wamesisitiza kuwa Marekani kamwe haitoichukua Greenland na kuitaka Washington kuheshimu hadhi ya mipaka inayotambuliwa kimataifa.

Nuuk | Kisiwa cha Greenland
Trump amesema kukichukua kisiwa cha Greenland ni muhimu kwa usalama wa Marekani.Picha: Mads Claus Rasmussen/Ritzau Scanpix/picture alliance

Matamshi ya viongozi hao yanafuatia hatua ya Rais Donald Trump kumteua mjumbe maalamu wa Washington kwa ajili ya Greenland na kuendelea kushinikiza umuhimu wa Marekani kuchukua udhibiti wa kisiwa hicho cha bahari ya Aktiki.

Waziri Mkuu wa Denmark  Mette Frederiksen na mwenzake wa Greenland Jens-Frederik Nielsen, wamesema kwenye tamko la pamoja jana Jumatatu kuwa kisiwa hicho kamwe hakitokwenda mikononi mwa Marekani na kupuuzilia mbali hoja za Washington kuhusu suala la usalama.

Trump amesema mara kadhaa kwamba angetamani Marekani ikinyakue kisiwa hicho kwa sababu za kiusalama, matamshi ambayo mara zote yamezusha ukosoaji mkubwa kutoka kwa Denmark, iliyo mshirika wa Washington.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW