Denmark yasitisha msaada kwa Tanzania
15 Novemba 2018Denmark ambayo ni nchi ya pili kwa ufadhili kwa Tanzania itazuwia sehemu kubwa ya fedha za misaada inayotoa kwa nchi hiyo kutokana na wasiwasi wa ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na matamshi ambayo hayakubaliki ya chuki dhidi ya binadamu wengine yaliyotolewa na afisa wa serikali.
Hayo yameelezwa na waziri wa misaada ya maendeleo wa Denmark bungeni jana. Waziri wa ushirikiano wa maendeleo Ulla Tornaes ameeleza kwamba ana wasi wasi mkubwa kuhusu hali hasi inayojitokeza nchini Tanzania, hususan matamshi ya chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, yaliyotolewa na mkuu wa mkoa.
Shirika la habari la Reuters lilisema kuwa halikuweza kuzungumza na maafisa wa serikali ya Tanzania ili kutoa maelezo yao kuhusu suala hilo.